SAKAJA ATANGAZA UPANUZI WA BOMBA LA MAJI TAKA KAUNTI YA NAIROBI
Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja ametangaza mradi kabambe unaoongozwa na Kampuni ya Majisafi na Majitaka ya Jiji la Nairobi (NCWSC) kupanua njia za kupitishia maji taka katika maeneo muhimu jijini.
Mpango huu unalenga kuimarisha huduma za usafi wa mazingira na kuhudumia idadi ya watu inayoongezeka jijini, ambayo inazidi watu milioni tano kila siku.
Wakati wa ziara ya hivi majuzi ya Makongeni, Eastleigh, na Kawangware, Mwenyekiti wa NCWSC Arnold Karanja amesisitiza hitaji muhimu la mradi huu, Chini ya uongozi wa Gavana Sakaja
Mipango inaendelea ya kupanua njia za maji taka ndani ya Wilaya ya Biashara ya Kati ya Nairobi (CBD), ikijumuisha karibu na eneo la Mahakama ya Juu.
Upanuzi huu ni sehemu ya mpango mpana wa kufanya mfumo wa maji taka wa jiji kuwa wa kisasa.
Imetayarishwa na Janice Merete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































