JULIUS YEGO ANAZIDI KUTAMBA
Bingwa wa zamani wa dunia Julius Yego alinakili urushaji wake bora msimu huu aliporusha mkuki kwa umbali wa mita 87.72 na kumaliza wa tano katika fainali ya kurusha mkuki kwa wanaume ambayo ilishindwa na Arshad Nadeem wa Pakistan na rekodi mpya ya Olimpiki ya mita 92.97 jana usiku.
Yego mshindi wa medali ya fedha 2016 alisema Olimpiki ya Paris ndiyo ilikuwa safari bora zaidi kwake licha ya kukosa kumaliza jukwaani.
Bingwa huyo wa dunia wa 2015 hata hivyo alionya Kenya itasalia nyuma iwapo mambo yataendelea kama kawaida.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































