AFARIKI KWA DAU YA MIA TATU HUKO KIRINYAGA

Mwanamume mwenye umri wa miaka 25 amekufa maji katika Eneo Bunge la Mwea, Kaunti ya Kirinyaga, alipokuwa akijaribu kuogelea katika bwawa la Mamlaka ya Kitaifa ya Umwagiliaji ili kushinda dau la shilingi 300.
Kelvin Gitonga, muogeleaji na mwendeshaji bodaboda maarufu huko Ngurubani, anadaiwa kuweka dau na rafiki yake kwamba angeweza kuogelea kutoka upande mmoja wa bwawa hadi mwingine hatu iliyopelekea kuzama kwake.
Imetayarishwa na Janice Marete