#Local News

MNYAMA ASIYEFAHAMIKA ALETA JOTO LIKUYANI

Wakazi wa Kijiji cha Lugulu eneo bunge la Likuyani kaunti ya Kakamega wanaishi kwa hofu kutokana na madai kwamba wamemwona mnyama asiyefahamika ikivamia mifugo wao.

Wakizungumza na wanahabari, wakazi hao wamesema kwamba hofu hiyo imeathiri masomo huku wakihofia usalama wa wanao wanapoelekea shuleni.

Aidha, wameitaka idara ya wanyamapori nchini KWS kuingilia kati na kumnasa mnyama huyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *