WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA MBEGU HALALI

Katika juhudi za kuimarisha uzalishaji wa chakula nchini, wakulima wamehimizwa kutumia mbegu kutoka kwa kampuni zilizoidhinishwa na bodi ya udhibiti na ubora wa mbegu KEPHIS.
Akizungumza katika kaunti ya Meru, mkurugenzi wa ubora wa mbegu nchini Simon Maina amesema kuwa serikali ina kesi 15 mahakani kuhusiana na mbegu ghushi, kesi 5 miongoni mwao zikiwa katika kaunti ya Meru.
Naye afisa mkuu wa kilimo kwenye kaunti hiyo James Mutia amewataka wakulima pia kuhakikisha mbegu za miche ikiwemo maembe zimeidhinishwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa