#Local News

GACHAGUA AMLAUMU RUTO KWA KUKATAA NYACHAE KUWA MWENYEKITI WA IEBC

Mjadala kuhusiana na uteuzi wa mwenyekiti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wazidi kupamba moto, baada ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kudai kuwa Rais William Ruto alipinga uteuzi wa Charles Nyachae na badala yake kumchagua Erastus Ethekon.

Gachagua amesema kuwa jopo la uteuzi lilikuwa limewasilisha majina ya Nyachae na Ethekon kwa Rais, lakini kwa madai ya uhasama wa zamani kati ya Ruto na familia ya Nyachae, jina lake likakataliwa huku akidai kuwa chaguo hilo linamlenga kumpendelea Rais Ruto katika uchaguzi wa 2027, kwa kuwa Ethekon anahusishwa kwa karibu na Naibu Mkuu wa Wafanyakazi wa Ikulu, Josphat Nanok.

Wakati huo huo, Gachagua ameeleza kuwa anaendelea kujipanga upya kwa uchaguzi wa 2027 na ameungana na viongozi wa upinzani kama Fred Matiang’i, Kalonzo Musyoka, Martha Karua, na Eugene Wamalwa.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *