POLISI KUIMARISHA OPERESHENI MATUNGU, KIRINYAGA
Wakazi wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na utovu wa usalama wanatarajia kupata afueni kufuatia hakikisho la serikali kutangaza operesheni maalum katika maeneo hayo kwa lengo la kukabili magenge ya kihalifu.
Baadhi ya maeneo hayo ni Kerugoya na Ngurubani kaunti ya Kirinyaga, Matungulu na Matungu kaunti za Machakos na Kakamega mtawalia.
Hata hivyo, akizungumza akiwa katika bunge la seneti kujibu maswali yaliyoibuliwa na maseneta, Murkomen ameahidi hatua Madhubuti kuchukuliwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































