#Sports

KOCHA MUFUTU ATOA ONYO KALI KWA KIKOSI CHAKE

KOCHA Mkuu wa Ulinzi Warriors, Bernard Mufutu ametoa onyo kali kwa kikosi chake dhidi ya kuzembea katika Ligi ya Kitaifa ya Mpira wa Kikapu (KNBL), kufuatia wikendi ya uchezaji tofauti.

Wanajeshi hao walipoteza kwa vikapu 70-68 kwa mabingwa watetezi Nairobi City Thunder siku ya Ijumaa, kabla ya kurejea na ushindi wa 81-65 dhidi ya Eldonets Platinum siku ya Jumapili. Ulinzi alianza kwa kusuasua, na kupoteza robo ya kwanza 17-24, lakini akavuma kwa kishindo katika kipindi cha pili kwa matokeo ya 29-9 na kutinga muda wa mapumziko na kuongoza 4-3.

Wanajeshi hao walidumisha kasi yao katika robo ya tatu, kwa kuwalaza Eldonets 16-12, kabla ya kupoteza kwa kiasi kidogo robo ya mwisho 19-20, kiasi cha kutosha kupata ushindi mnono wa 81-65.

Elisha Odhiambo aliongoza kutoka mbele kwa pointi 19, huku David Kitongo, Collins Muliro, na Simon Rapudo wakiwa na pointi 37 na kuwawezesha Ulinzi kupata ushindi.

Kwa upande mwingine, Clifford Mumbo na Neville Otieno walijitokeza kwa Eldonets, wakichangia pointi 20 na 18 mtawalia.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KOCHA MUFUTU ATOA ONYO KALI KWA KIKOSI CHAKE

BUNGOMA QUEENS WAINGIA FAINALI

KOCHA MUFUTU ATOA ONYO KALI KWA KIKOSI CHAKE

UAJIRI SHA WAPIGWA BREKI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *