RAIS ASHTUMU KIFO CHA OJWANG
Rais William Ruto ameshtumu kifo cha mwanablogu Albert Ojwang akisema waliohusika wanastahili kuchukuliwa hatua pasipo kuzingatia cheo wanachoshikilia.
Rais ameitaka idara ya polisi kushirikiana na mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisi Ipoa katika uchunguzi kwenye kifo hicho akisema polisi wana jukumu la kulinda usalama na maslahi ya washukiwa wanapokamatwa.
Imetayarishwa na Maureen Amwai
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































