RUTO AAGIZA NYS KUWASAJILI WATU 20,000 MWAKA UJAO
Rais William Ruto ameagiza Huduma ya Vijana kwa taifa (NYS) kuongeza idadi ya walioajiriwa hadi 20,000 katika uhudumu wao ujao.
Akizungumza alipoongoza gwaride la kufuzu kwa makurutu wa NYS huko Gilgil, Ruto amesema kundi la mwaka huu lilikuwa karibu watu 15,000 na anafurahia hilo.
Alisema serikali itahakikisha vijana wengi zaidi wananufaika na mafunzo yanayotolewa na NYS.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































