#Local News

MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KUHUSU INSPEKTA MKUU WA POLISI GILBERT MASENGELI

Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi wa iwapo itakumbatia uamuzi wake wa juma iliyopita wa kumhukumu naibu inspekta mkuu wa polisi katika kitengo cha polisi wa utawala Gilbert Masengeli, hii ni baada ya Masengeli kukabiliwa na maswali mahakamani akitakiwa kueleza ni kwanini alikaidi agizo la mahakama la kumtaka afike mbele yake kuhusiana na kutekwa nyara kwa ndugu wawili na mwana harakati alipokuwa akihudumu kama kaimu inspekta generali wa polisi.

Hakimu mkuu Lawrence Mugambi Anatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi hiyo leo mwendo wa saa kumi

Mahakama pia imemuamuru Masengeli kuwepo mahakamani wakati maamuzi ya mwisho itapotolewa. Mapema leo asubui, Masengeli aliomba msamaha kwa mahakama iliyompata na hatia ya kupuuza kufika kwenye vikao vya koti kutoa maelezo

Masengeli ambaye amekuwa akihudumu kama kaimu inspekta mkuu wa polisi, alihukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani ila kifungo hicho kikafutiliwa mbali kwa siku 7 ili kumwezesha ajiwasilishe mahakamani.

Licha ya kutaja majukumu ya kikazi kuwa sababu za kukosa kufika mahakamani, Masengeli ameahidi kutii sheria na kushirikiana na mahakama siku zijazo.

Imetayarishwa na Kennedy Osoro

MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KUHUSU INSPEKTA MKUU WA POLISI GILBERT MASENGELI

GACHAGUA ASIMULIA TUMAINI JIPYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *