#Business

KENYA YALENGA KUONGEZA MAUZO YA CHAI KUFIKIA 2030

Wakulima wa zao la chai watanufaika na mpango mpya wa serikali kupitia Wizara ya Kilimo wa kuongeza mauzo ya chai ya Kenya kwenda China kwa zaidi ya mara nne ifikapo mwaka 2030.

Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mutahi Kagwe, amesema lengo ni kuongeza mauzo kutoka kilo milioni 12.42 mwaka 2024 hadi kilo milioni 50, hatua itakayoongeza mapato kwa wakulima na kukuza uchumi wa kilimo.

Kagwe alitoa tangazo hilo baada ya kikao na Zhang Chaobin, mwenyekiti wa kampuni ya Fuzhou Benny Tea Industry kutoka China, mjini Nairobi, katika juhudi za kuimarisha ushawishi wa Kenya kwenye soko la chai la China.

Imetayarishwa na Maureeen Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *