#Local News

PENZI LA MAUTI

Polisi katika Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja na watoto wake watatu waliteketezwa ndani ya nyumba yao huko Manyatta kando ya barabara kuu ya Kisumu Nairobi.

Mshukiwa huyo wa uchomaji moto anasemekana kufunga mlango kwa nje kabla ya kuchoma jengo la Mabati kwa kutumia petroli wakati wa tukio hilo la saa 2 asubuhi.

Nyumba zingine kumi zilizo karibu pia ziliteketea huku wakaazi wakipoteza mali zao zote licha ya juhudi za idara ya zima moto Kisumu kuzima moto huo.

Majirani waliofadhaika asubuhi ya leo wamesimulia matukio yaliyosababisha kitendo hicho kiovu wakisema wanashuku kisa hicho kilichochewa na mzozano wa kimapenzi

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *