UTEUZI WA TUME

Wakenya 6 zaidi wanahojiwa hii leo katika kinyang’anyiro cha kujaza nafasi za makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.
Miongoni mwa walihojiwa tayari hii leo ni wakili Mary Kigen, ambaye ameahidi kutumia ujuzi wake wa kisheria kuboresha utendakazi wa IEBC.
Haya yanajiri huku waziri mteule wa utumishi wa umma Geoffrey Ruku na mwenzake wa jinsia Hannah Wendot Cheptumo wakiratibiwa kuhojiwa hii leo na kamati ya uteuzi ya bunge la kitaifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa