MAREKANI YAMSUTA RUTO

Waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Antony Blinken amemtaka Rais William Ruto kuheshimu mchango wa vijana katika maendeleo ya taifa la Kenya, akisisitiza umuhimu wa vijana kuruhisiwa kujieleza kupitia maandamano kisheria.
Katika mazungumzo ya simu baina ya wawili hao, Blinken aidha ameponegeza hatua ya Ruto kuiagiza mamlaka huru ya kuchunguza mienendo ya maafisa wa polisi IPOA kuwawajibisha maafisa wa polisi waliokiuka sheria wakati wa maandamano.
Aidha, wawili hao wamezungumza kuhusu masuala ya polisi wa Kenya kuongoza operesheni ya kurejesha utulivu nchini Haiti.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa