#Sports

KENYA NDO WASHINDI WA KABADDI

Kenya ilinyakua taji la Ubingwa wa Afrika Kabaddi 2024 Jumamosi jioni baada ya kulaza Uganda 44-23 katika mechi ya mwisho ya msururu huo ulioandaliwa Kasarani.

Kenya ilianza mechi kwa nguvu huku James Kamweti akizalisha mashambulizi kadhaa katika nusu ya Uganda na kuiweka Kenya mbele wakati wa mapumziko kwa alama 20-13.

Ushindi huo unamaanisha kuwa Kenya itashiriki Kombe la Dunia lijalo la Kabaddi.

Kamweti, ambaye pia alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi baada ya kuonyesha kiwango kizuri, alijigamba kuwa Kenya ni wababe wa Afrika mjini Kabaddi baada ya ushindi huo mnono.

Nahodha wa Kenya David Silishia aliimwagia sifa timu hiyo akisema tayari wanatazamia Kombe la Dunia.

Mkenya Samuel Wafula alitajwa kuwa beki bora wa michuano hiyo.

Mafanikio ya Kenya katika Mashindano ya Afrika ya Kabaddi yanaongeza mafanikio yao ya hivi majuzi ya kupata medali ya shaba katika Kombe la Bangabandhu nchini Bangladesh, na kuonyesha umashuhuri wao unaokua katika jamii ya kimataifa ya Kabaddi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KENYA NDO WASHINDI WA KABADDI

UHISIPANIA WAINGIA ROBO FAINALI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *