SERIKALI YATANGAZA TAREHE MPYA YA LIKIZO FUPI KWA WANAFUNZI
Wizara ya Elimu imefanya marekebisho ya tarehe za likizo fupi ili kufidia muda wa masomo uliopotea wakati shule zikilazimika kufungwa kutokana na mafuriko.
Kufuatia mabadiliko hayo, yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa Elimu Dkt Belio Kipsang Jumatano, wanafunzi wa chekechea, shule za msingi na upili wanatarajiwa kuelekea likizo fupi kuanzia 26 hadi 28 Juni mwaka huu.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































