OMANYALA AORODHESHWA KATIKA NAFASI YA PILI KWENYE JEDWALI YA WANARIADHA WENYE KASI ZAIDI DUNIANI.

Ferdinand Omanyala ameorodheshwa katika nafasi ya pili ulimwenguni msimu huu kwenye jedwali la wanariadha wenye kasi zaidi duniani.
Omanyala alishinda mbio za mita mia moja jijini Brussels Ubelgiji katika mashindano ya Diamond League kwa kuandikisha muda wa sekunde 10.07.
Baada ya msimu wa msururu wa mbio za mwaka 2024, Omanyala ametua katika nafasi ya pili kwa kuandikisha muda bora wa msimu ya wastani ya sekunde 9.79.
Mwanariadha wa Jamaica Kishane Thompson ndiye bingwa na aliandikisha muda bora wa msimu kwa kuweka rekodi ya sekunde 9.77.
Katika nafasi ya pili, Omanyala alifuatana na bingwa wa Olimpiki ya 2024 jijini Paris, Ufaransa Noah Lyles.
Katika nafasi ya 4 ni Fred Kerly wa Marekani, akifuatiwa na Oblique Seville wa Jamaica, kisha Akani Sambine wa Afrika Kusini na saba bora ikifungwa na Marcell Jacobs wa Italia.
Katika mbio za mita 800, Emmanuel Wanyonyi anaongoza jedwali hilo kwa kuandikisha muda bora wa msimu, Aaron Kemei ameorodheshwa katika nafasi ya saba akifuatiwa na Wyclife Kinyamala.
Kwa upande wa kina dada Faith Kipyegon anaongoza kwa muda bora wa msimu akifuatiwa na Gudaf Tsegay wa Ethiopia.
Imetayarishwa na Kennedy osoro