LIVERPOOL YAPOTEZA 3-2 DHIDI YA FULHAM

Liverpool ilikubali kipigo cha pili msimu huu baada ya Fulham kushinda 3-2, huku Southampton ikishushwa daraja kwa kufungwa 3-1 na Tottenham.
Sare ya 1-1 ya Arsenal na Everton ilifanya Liverpool kuhitaji pointi 11 ili kushinda taji la 20 la ligi kuu ya Uingereza.
Baada ya Alexis Mac Allister kufunga, ulinzi mbovu uliruhusu Fulham kubadili matokeo kupitia Ryan Sessegnon, Alex Iwobi na Rodrigo Muniz.
Liverpool bado ina nafasi nzuri ya kushinda taji lao la kwanza tangu 2020, licha ya kipigo hicho.
Imetayarishwa na Janice Marete