WALIMU 46,000 WAPATA AJIRA YA KUDUMU, TSC

Walimu wote 46,000 wa shule za sekondari msingi JSS wamepata afueni baada ya tume ya kuwaajiri walimi TSC kutangaza kuwapa ajira za kudumu kuanzia Januari mwaka ujao, huku mchakato wa kuwapandisha vyeo walimu zaidi ukiendelea.
Haya ni kwa mujibu wa afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Nancy Macharia, ambaye ameiambia kamati ya elimu katika bunge la kitaifa kwamba walimu 46,000 hao wamechaguliwa kutoka kwa maombi 314,117 yaliyokuwa yametumwa.
Kati ya maombi hayo, 144,177 yalitoka kwa walimu wa JSS, huku 39,950 pekee wakichaguliwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa