GAVANA IRUNGU, VIJANA WAKUTANA

Gavana wa Laikipia Joshua Irungu amefanya kikao na vijana kutoka sehemu mbali mbali kwenye kaunti hiyo kwa lengo la kufahamu kinachowakera kwenye serikali yake.
Wakizungumza baada ya kikao hicho, vijana hao wamesema watashirikiana na serikali iwapo maoni yao yatasikilizwa na kutekelezwa, wakilalamikia ukosefu wa kazi na uwazi katika serikali hiyo.
Laikipia ni mojawapo ya kaunti ambazo ziliathirika pakubwa na uharibifu wa mali wakati wa maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa