MMOJA AUAWA KIMILILI, NYUMBA ZABOLEWA
Hali ya kawaida imeanza kurejea katika kijiji cha Kibingei eneo bunge la Kimilili kaunti ya Bungoma baada ya polisi kuwakamata washukiwa watatu kufuatia mauaji ya mwanamme mwenye umri wa miaka 34 eneo hilo kuhusiana na kinachoaminika kuwa mzozo wa kimapenzi.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi eneo la Kimilili Nzaka Mwitu, mwathiriwa kwa jina Ben Kisabuli alishambuliwa alipokuwa akiekea nyumbani na kujeruhiwa kabla ya kuaga dunia alipokuwa akitibiwa.
Hata hivyo, watu wasiojulikana walibomoa nyumba za washukiwa kwa lengo la kulipiza kisasi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































