NAKHUMICHA ASEMA MSWADA UMEATHIRI SHIF

Waziri wa afya Susan Nakhumicha ametangaza kwamba wakenya watakuwa na uwezo wa kujisajili katika mpango wa afya ya jamii SHIF kuanzia tarehe 1 Julai kupitia tovuti ya mamlaka ya afya ya kijamii.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Nakhumicha amesema wizara yake inafanya marekebisho kuhusiana na hazina mbali mbali za afya ikiwemo ile ya matibabu ya dharura na afya ya kimsingi, baaada ya mswada wa fedha kuondolewa.
Aidha, amewahakikishia wakenya ambao wamekuwa kwenye mpango wa NHIF kwamba wataendelea kupata huduma za kimatibabu chini ya mpango mpya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa