POLENI WALIMU
Ni pigo kubwa kwa Walimu baada ya Tume ya Kuajiri Walimu kusema kuwa haitakuwa na uwezo wa kutekeleza nyongeza ya mishahara inayotarajiwa kutokana na kupunguzwa kwa bajeti ya Shilingi 10
Walimu pia watakuwa wakifanya kazi bila bima ya matibabu kuanzia Desemba wakati uhalisia wa marekebisho ya bajeti unapoanza.
Walimu 46,000 waliohitimu watasubiri kwa muda mrefu zaidi kujiunga na orodha ya malipo ya serikali katika mabadiliko mapya ambayo tume imeweka kujibu mapendekezo ya bajeti.
Afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia akizungumza mbele ya bunge jana jumatano amesema kuwa walimu watalazimika kusubiri kwa muda mrefu kwani kuheshimu makubaliano ya pamoja ni jambo lisilowezekana.
Awamu ya pili ya 2021-25 iliyorekebishwa mkataba wa makubaliano CBA ulipaswa kutekelezwa mwishoni mwa mwezi huu. Haya ni kwa mujibu wa makubaliano kati ya tume hiyo na miungano ya walimu.
Awamu ya kwanza ilianza Julai 1, 2023 hadi Juni 30, 2024.
Walimu walipaswa kupata posho za nyumba zilizoboreshwa, hasa kwa wale walio katika nguzo ya nne. Pia walipaswa kufaidika kutokana na ongezeko la mapato ili kuwaepusha na kupanda kwa gharama ya maisha.
Ongezeko la mishahara lilikuwa kugharamia walimu wote walioajiriwa kabla ya Julai 1, 2023.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































