WAWILI WASHTAKIWA KWA MAUAJI ELDORET
Watu wawili wanaodaiwa kumuua mwanamume wa makamo miezi kadhaa iliyopita kwa kushukiwa kuwa jambazi wameshtakiwa kwa mauaji katika mahakama kuu ya Eldoret.
Robert Kiplagat, mkulima mdogo na Alex Kiptoo, mwanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Udaktari cha Kenya (KMTC) katika chuo kikuu cha Nairobi walipofika mbele ya Jaji Robert Wananda wakukanusha shtaka moja la mauaji.
Mahakama iliyojaa watu ilisikia kwamba walitenda kosa hilo mnamo Aprili 6, 2024, eneo la HZ Keiyo Kusini, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































