OBADO BADO KIKAANGONI

Mahakama kuu imeipa ruhusa tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC kuipiga mnada mali ya thamani ya shilingi milioni 235 ya aliyekuwa gavana wa Migori Okoth Obado, anayokisiwa kuipata kupitia njia za udanganyifu.
Miongoni mwa mali hiyo ni nyumba za makazi katika mtaa wa Loresho jijini Naiorbi na magari mawili ya kifahari, ambayo EACC inasema zinatokana na ufujai wa fedha katika serikali ya kaunti ya Migori chini ya uongozi wa Obado.
Amri ya mahakama imetolewa na hakimu Esther Maina, baada ya Obado na EACC kukubaliana kupata suluhu nje ya mahakama.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa