WADHIFA ULIOBAKI KWENYE BARAZA WAWANIWA
Muungano wa watu walio na changamoto za kimaumbile wamemtaka Rais William Ruto kumteua mmoja wao kuwa Waziri wa masuala ya jinsia na torathi za kitaifa, wakisema wametamaushwa kutokana na ukosefu wa mmoja wao kuteuliwa katika baraza la mawaziri.
Kwenye kikao na wanahabari, muungano huo umemtaka RAis kuhakikisha usawa wa uwakilishi kuambatana na katiba ya Kenya.
Aidha, wamesema kuwa kuna watu wengi walio na changamoto za kimaulbile ila wana uwezo wa kuiongoza wizara hiyo.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































