“HATULIPI HIYO!” BODA BODA WAPINGA ADA

Wahudumumu wa boda boda kaunti ya Nandi wamefanya maandamano kulalamikia kurejeshwa kwa ada ya kuegesha pikipiki mjini Kapsabet, muda mfupi baada ya maafisa wa manispaa ya kaunti hiyo kunasa pikpiki kadhaa ambazo hazikuwa na nembo ya kaunti.
Wahudumu hao wameelekea hadi katika za maafisa hao wakitaka kujua sababu ya kunaswa kwa pikipiki za wenzao, licha ya agizo la gavana Stephen Sang kwamba ada hiyo isitozwe.
Hata hivyo, mawaziri wa fedha na utawala wa kaunti hiyo wameahidi kuondolewa kwa ada hiyo baada ya kikao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa