KAMATI YA FEDHA YAPENDEKEZA KIFUNGU TATA NJE
Kamati ya fedha katika bunge la kitaifa imelitaka bunge hilo kutupilia mbali kipengee chenye utata kwenye mswada wa kifedha wa 2025-26 kinacholenga kuipa mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA uhuru wa kuingilia deta za kibinafsi za walipa ushuru.
Kipengee hicho cha 52 kwenye mswada huo kinapendekeza sheria ya ukusanyaji ushuru kufanyiwa marekebisho ili kuondoa kizuizi dhidi ya KRA kupata deta hizo.
Miongoni mwa deta hizo ni taarifa za kifedha kupitia njia za sim una benki, KRA ikilenga kutumia mfumo huo ili kudhibiti ukwepaji wa kulipa ushuru.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































