#Local News

AULIWA KWA SHOKA AKIJARIBU KUTENGANISHA VITA BAINA YA WANANDOA

Mwanamume mwenye umri wa miaka 28 amekatwa kwa shoka hadi kufa alipojaribu kutenganisha wanandoa waliokuwa wanapigana katika kijiji cha Buyinje, Musoli, Kaunti ya Kakamega.

Marehemu ametambulika kwa jina la Moses Akumali.

Mashahidi wamesema alikuwa akielekea nyumbani aliposhuhudia wanandoa wakipigana ndipo Kchukua uamuzi wa kuingilia kati ili kusitisha mapigano.

Haijabainika ni nini kilisababisha mabishano na mapigano kati ya wanandoa hao.

Wanakijiji walimuokoa majeruhi na kumpeleka katika Hospitali moja eneo hilo ili kupata matibabu
kulingana na polisi, hali yake ilidhoofika, na kuaga dunia alipokuwa akikimbizwa katika hospitali ya nyingine Kaunti ya Kakamega.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti ukisubiri uchunguzi .

Imetayarishwa na Janice Marete

AULIWA KWA SHOKA AKIJARIBU KUTENGANISHA VITA BAINA YA WANANDOA

WAFANYAKAZI WA ANGA KATIKA JKIA WAANDAMANA

AULIWA KWA SHOKA AKIJARIBU KUTENGANISHA VITA BAINA YA WANANDOA

KUPPET YAENDELEA KULEMAZA MASOMO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *