RUTO AKUTANA NA MAWAZIRI

Rais William Ruto anafanya kikao na baraza la mawaziri, wakati ambapo wengi wa mawaziri wake wanalaumiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao, mbali na kujihusisha na ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma.
Kikao cha rais kimethibitishwa na msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed.
Katika kikao cha seneti hapo jana, maseneta walitumia fursa hiyo kuwakosoa baadhi ya mawaziri na maafisa wakuu serikalini.
Samson Cherargei ni seneta wa Nandi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa