#Local News

PPB YAENDESHA ‘MSAKO WA AFYA BORA’

Wakenya wanatarajia kuimarika kwa ubora wa dawa na usalama wa afya yao kufuatia msako unaofanywa na bodi ya sumu na dawa nchini dhidi ya usambazaji wa dawa haramu kwenye maduka ya dawa na wahudumu wengine wa afya.

Msako huo unaendeshwa kwa ushirikiano na idara ya polisi ukiwalenga wawasilishaji wa vifurushi ama parcels na wasafirishaji mizigo wasio na leseni ya kusambaza dawa.

Kwa mujibu wa afisa anayesimamia msako huo Julius Kalwayi, lengo kuu ni kudhibiti maduka ya dawa yasiowafuata sheria.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *