KENYA KUANGAZIA UPYA MARUFUKU YA MITUMBA

Serikali ya Kenya inawazia kupiga marufuku uagizaji wa mitumba ili kufufua sekta ya ushonaji nchini, Wizara ya Biashara ikisema kuwa mitumba imedhoofisha viwanda vya nguo vya ndani.
Kati ya mwaka 2019 hadi 2023, Kenya iliagiza mitumba ya thamani ya KSh 95.2 bilioni, huku kiwango kikiongezeka kwa asilimia 11.5 mwaka 2023 pekee.
Hata hivyo, marufuku hiyo huenda ikazorotesha uhusiano wa kibiashara na Marekani, ambayo tayari imeweka ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za Kenya.
Wizara sasa inapanga kudhibiti uagizaji na kuimarisha uzalishaji wa ndani, japo bado hakuna uamuzi wa mwisho.
Nchi za Rwanda, Uganda na Ethiopia tayari zimechukua hatua hiyo na kupiga marufuku uagizaji wa mitumba.
Imetayarishwa na Mercy Asami