WANAFUNZI ELFU 153 PEKEE WASAJILIWA NA KUPCCS

Maswali yanaendelea kuibuliwa baada ya wanafunzi takribani elfu 60 walioafikia vigezo vya kutuma maombi ya usajili katika vyuo vikuu nchini kupitia taasisi ya usajili wa wanafunzi katika vyuo KUPCCS kukosa kufanya hivyo mwaka huu.
Kwa mujibu ya KUPCCS wanafunzi elfu 153 pekee ndio wamefanikiwa kuwasajili katika vyuo vikuu vya umma na vya kibinafsi huku elfu 10 na mmoja ambao waliafikia hitaji la kufanya kosi za degrii wakijisajili kufanya kosi za diploma miongoni mwa elfu 153elfu 75,714 watafanya kosi za uwalimu kwenye vyuo vikuu huku elfu 10263wakijiunga na vyuo vya uawalimu TTC’S na kwa mara ya kwanza KUPCCS imewasajili wanafunzi elfu 19653 katika taasisi ya mafunzo ya utabibu KMTC kupitia mpango huo.
Usajili wa mwaka huu unawakilisha asilimia ndogo sana ikilinganishwa na nafasi za masomo zilizopo katika vyuo vikuu , vya kiufundi na taasisi nyingine.
Mwaka huu kulikuwa na nafasi milioni moja za kosi mbali mbali kupitia KUPCCS.
Wale ambao hawakuridhika na kozi ambazo wamechaguliwa kuzifanya wana nafasi ya kuchagua kozi nyingine kwazia mwezi ujao wa juni huku wale ambao wameridhika wakitakiwa kutuma maombi ya kupata ufadhili wa HELB.
Imetayarishwa na: Janice Marete