ECHOES OF WAR: WANAFUNZI WA BUTERE GIRLS WASUSIA

Hamu ya wanafunzi wa Butere Girls kuonyesha uwezo wao wa kuigiza imezimwa mapema leo, kufuatia uamuzi wao kususia kuigiza mchezo wenye utata wa Echoes of War ulioandikwa na aliyekuwa seneta wa Kakamega Cleophas Malala.
Wanafunzi hao ambao wamenyimwa kipaaza sauti walipokuwa jukwani mbali na wananchi kuzuiwa kuingia kwenye ukumbi, badala yake wameimba wimbo wa taifa na kuondoka jukwaani, wakisema hawajakuwa wakifanya mazoezi wala kukutana na waelekezi wa mchezo huo kwa wiki 3 zilizopita.
Echoes of War ilipigwa marufuku wakati wa mashindano ya michezo ya kuigiza ukanda wa Magharibi mwa nchi kabla ya mahakama kuu kuamuru kwamba ijumuishwe kwenye mashindano ya kitaifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa