#Sports

CECAFA YA WANAWAKE KUANZA MWEZI HUU

Mashindano ya CECAFA kwa Wanawake 2025 yamepangwa rasmi kuanzia Juni 12 hadi 22 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Kwa mujibu wa Yusuf Mossi, Mkurugenzi wa Mashindano katika Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), uamuzi wa kuandaa michuano hiyo kabla ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake la CAF (WAFCON) ulikuwa wa kimkakati.

Mataifa manne ambayo ni wenyeji Tanzania, Uganda, Burundi na Sudan Kusini yamethibitisha kushiriki huku timu zaidi zikitarajiwa kujiunga na vikosi hivyo siku chache zijazo.

Baada ya michuano hiyo ya wanawake, CECAFA pia itaanda kwa mara ya kwanza mashindano ya soka la ufukweni ya CECAFA, ambayo imepangwa kufanyika Julai 7 hadi 12 mjini Mombasa, Kenya.

Kalenda ya CECAFA yenye shughuli nyingi ya 2025 pia inajumuisha mechi za kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika ya CAF ukanda wa CECAFA na Kombe la Dar Port Kagame, zote zikifanyika Tanzania, pamoja na kufuzu kwa AFCON U-17 nchini Ethiopia. Michuano ya kikanda ya kufuzu kwa Michuano ya Soka ya Shule za Afrika ya CAF pia iko kwenye ajenda.

Hata hivyo, matukio mawili makubwa, Kombe la Chalenji la CECAFA na Mashindano ya CECAFA U-20 kwa Wanawake, hayatafanyika mwaka huu.

Imetayarishwa na Nelson Andati

CECAFA YA WANAWAKE KUANZA MWEZI HUU

JADON SACHO AREJEA MACHESTER UNITED

CECAFA YA WANAWAKE KUANZA MWEZI HUU

NANE WAFARIKI KWENYE AJALI MWINGI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *