#Business

KENYA YAONDOA IMF KWENYE BAJETI

Kenya imejitoa katika kupata fedha kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwenye bajeti yake inayokuja, itakayoanza Julai mwaka huu. Hatua hii inaashiria jitihada za kuepuka masharti magumu ya IMF kama vile ongezeko la ushuru, kufungiwa ajira, na kupunguzwa kwa matumizi ya serikali.

Hati za bajeti zilizowasilishwa bungeni zinaonyesha kuwa hakuna fedha kutoka IMF zitakazotengwa hadi mwaka 2029, huku ikiwa imepungua kutoka Shilingi bilioni 135.1 zilizopokelewa mwaka wa kifedha wa 2023/24 na Shilingi bilioni 50.2 zilizopangwa awali kwa mwaka 2024/25.

Imetayarishwa na Mercy Asami

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *