RUTO ATETEA ADANI

Azma ya kampuni ya Adani ya India kupata kandarasi ya kujenga nguzo za kusambaza umeme humu nchini imepigwa jeki baada ya Rais William Ruto kutetea mpango wa serikali kuipa kandarasi hiyo ya mabilioni ya pesa, akisema inaondolea serikali mzigo wa kukopa fedha zaidi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kuchimba nishati kutumia mvuge eneo la Menengai kaunti ya Nakuru, Rais amezitaka kampuni za kibinafsi kuendelea kushirikiana na serikali ili kufanikisa miradi zaidi ya umma.
Aidha, Rais ametaja miradi ya kawi safi kuwa inayochangia ukuaji wa uchumi bila kuchafua mazingira.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa