#Sports

KIPA WA PSG AONYA KIKOSI CHAKE DHIDI YA KULEGEZA KAMBA

Mlinda mlango wa Paris Saint-Germain Gianluigi Donnarumma ameonya kwamba mabingwa hao wapya wa Ulaya wana uchu wa mafanikio zaidi katika Kombe la Dunia la Vilabu huku wakijiandaa kumenyana na Botafogo ya Brazil kesho asubuhi.

Miamba hao wa Ufaransa walizindua kampeni yao ya Kundi B kwa mtindo wa kuvutia siku ya Jumapili, wakiizaba Atletico Madrid mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Pasadena Rose Bowl.

Ushindi huo uliashiria azma yao ikiwa ni zaidi ya wiki mbili baada ya kuifunga Inter Milan mabao 5-0 kwenye fainali ya UEFA Champions League.

Donnarumma alisema timu hiyo inaangazia kwa dhati kushinda kombe la tano msimu huu baada ya kuanza mashindano “kama walivyomaliza” Ligi ya Mabingwa.

Imetayrishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *