#Football #Local News #Sports

GOR MAHIA ITAFUZU NUSU FAINALI YA CECAFA?

Mabingwa wa ligi kuu ya Kenya, Gor Mahia wanakabiliwa na kibarua kigumu hii leo wanapotarajiwa kumenyana na wababe wa ligi kuu nchini Sudan AI Hilal katika mchuano wao wa mwisho wa kundi B, ili kupata nafasi ya kufuzu kwa nusu fainali kwenye michuano ya Kagame Cecafa, kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya ASAS Djibouti Telecom katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Azam Complex jijini tanzania

KO’gallo alianza kufunga kupitia kwa Levin Odhiambo dakika ya 40, lakini Warsama Houssein akaijibu Telcom dakika ya 42.

Matokeo hayo yanawafanya Gor walioilaza 1-0 na Red Arrows ya Zambia katika mchezo wa kwanza wakiwa katika hali ya lazima

Hii ilikuwa mara ya pili kwa Gor kukutana na vijana hao wa Djibouti, baada ya kuwafunga mabao 3-1 katika mechi ya awali, nchini Tanzania mwaka 2015, walipotinga fainali ambapo walifungwa mabao 2-0 na Azam FC ya Tanzania.

KO’gallo wanashika nafasi ya tatu kwenye jedwali wakiwa na pointi moja, huku Arrows wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi tatu.

Telcom inafunga na point 1

Kocha mpya wa Gor Leonardo Neiva ambaye anaiongoza timu hiyo katika mgawo wake wa kwanza anasema timu hiyo ni kazi inayoendelea, na wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha falsafa yake ya uchezaji inaeleweka.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *