#Local News

MLIPUKO WA BETRI WAJERUHI MVULANA WA MIAKA 12, NA KUTEKETEZA NYUMBA 8 HUKO HOMA BAY

Mvulana mwenye umri wa miaka 12 amelazwa hospitalini akiwa na majeraha mabaya ya moto huku nyumba nane za kukodi zikiteketea na kuwa majivu baada ya betri kulipuka katika nyumba ya kupanga katika Kituo cha Biashara cha God Jope, Lambwe Magharibi, Kaunti ya Homa Bay.

Mvulana huyo amekimbizwa katika Kituo cha Afya cha Ogongo baada ya kuumia vibaya kwenye mkono wa kushoto alipokuwa akijaribu kukata umeme kutoka kwa betri.

Kaimu Chifu wa eneo la Lambwe Magharibi Fredrick Onyango Odero anasema betri hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na sola ililipuka na kusababisha moto huo wakati mvulana huyo alipokuwa akikata umeme.

Imetayarishwa na Janice Marete

MLIPUKO WA BETRI WAJERUHI MVULANA WA MIAKA 12, NA KUTEKETEZA NYUMBA 8 HUKO HOMA BAY

STARS WAZIMWA NYOTA NA CAMEROON

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *