HAKIMU STELLA ATAMBO APATA AFUENI YA MUDA
Mahakama Kuu imesitisha kwa muda kesi ya ufisadi dhidi ya Hakimu wa Thika, Stella Atambo, ikizingatia ombi la kupinga uhalali wa mashtaka hayo.
Atambo, kupitia mawakili wake, amedai kesi katika Mahakama Kuu na mahakama ya chini zinahusu masuala tofauti.
Chama cha Mahakimu na Majaji wa Kenya (KMJA) kimeonya kuwa uhuru wa mahakama uko hatarini, kikilaani unyanyasaji na vitisho dhidi ya maafisa wa mahakama, huku kikidai EACC inatumia vibaya mchakato wa kisheria.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































