WAKENYA: HATUTAKI MASHIRIKIANO NA ADANI TENA
Wakenya wameibua hisia mseto kuhusiana na hatua ya rais William Ruto kufutilia mbali mkataba wa kibiashara na kampuni ya adani.
Baadhi ya kina mama wametaja hatua hiyo kuwa ya kijasiri na ambayo imeonyesha ukomavu wa serikali kwa kuwa imebadilisha taswira ya serikali kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya wakenya wameeleza kuwa hatua ya rais Ruto haijatokana na ushawishi wa wakenya bali amechukua hatua hiyo kufuatia taarifa za kijasusi kutoka kwa mataifa ya kigeni.
Wakenya hao wanapendekeza rais Ruto pia kufutilia mbali bima mpya ya afya ya jamii SHA kwa kuwa kulingana nao adani inahusishwa na SHA.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































