#Local News

KANZE DENA ADAI KUTISHWA NA SERIKALI

Msemaji wa afisi ya Rais wa nne wa Kenya Kanze Dena, amedai kwamba wafanyakazi katika afisi hiyo ambayo ni ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta wanapokea vitisho.

Akiwahutubia wanahabari, Dena aidha amedai kwamba serikali imedinda kuwapa kandarasi mpya wafanyakazi wawili kwenye afisi hiyo, ambao ni msimamizi wa afisi George Kariuki na mkurugenzi wa mawasiliano Kanze Dena Mararo.

Huku akionekana kupinga madai ya msemaji wa serikali Isaac Maura, Dena amesema serikali haijakuwa ikiyarekebisha magari wala kuwapa mafuta.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *