#Local News

WAKAZI WA SUNA MAGHARIBI WALALAMIKIA UVAMIZI WA NYANI

Wakazi wa God Kweru, Suna Magharibi, Kaunti ya Migori, wanakadiria hasara kutokana na uvamizi wa nyani katika mashamba yao, hali inayowakatisha tamaa.

Kiongozi wa jamii, Timothy Odhiambo, amesema wakulima wengi wameacha kulima kwa hofu ya mazao yao kuharibiwa. Licha ya juhudi mbalimbali za kudhibiti tatizo hilo, hakuna suluhisho lililofanikiwa.

Wakazi hao wameshawasilisha malalamiko yao kwa serikali ya kaunti bila mafanikio na sasa wanataka fidia kwa hasara waliyoipata.

Imetayarishwa na Janice Marete

WAKAZI WA SUNA MAGHARIBI WALALAMIKIA UVAMIZI WA NYANI

MWANAUME AKAMATWA KWA KUMUUA BINAMU YAKE MIGORI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *