NYOTA YA STARS YAREJEA
Mabao mawili kutoka kwake John Avire na Duke Abuya Jumanne uliipa Harambee Stars ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji Namibia katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 kwenye Uwanja wa Orlando jijini Johannesburg, Afrika Kusini. .
Ushindi huo uliifanya Kenya kurejea kwenye mstari wa kampeni yake ya kufuzu kufuatia sare ya 0-0 dhidi ya Zimbabwe Ijumaa iliyopita katika mechi ya ufunguzi ya Kundi J iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda.
Alama hizo tatu ziliweka Harambee Stars hadi kileleni mwa kundi hilo kwa pamoja na Cameroon wenye pointi nne lakini Kenya inajivunia tofauti ya mabao.
Ushindi huo unamaanisha Harambee Stars inaongoza kundi J kwa pointi nne, sawa na Cameroon ambao walitoka sare tasa na Zimbabwe katika mechi ya awali.
Kenya itacheza na Cameroon wakati wa mapumziko ya kimataifa ya Oktoba katika mechi zitakazobainisha matokeo ya kundi hilo.
Vinara wa Kundi na washindi wa pili watafuzu kwa mashindano ya AFCON 2025 yaliyopangwa Morocco.
Mara ya mwisho Kenya ilifuzu kwa shindano la kwanza la bara ilikuwa 2019 nchini Misri.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































