UCHAGUZI WA KTDA NYAMIRA

Wakulima wa zao la majani chai katika kaunti ya Nyamira wameshauriwa kuwa makini na wale watakao wachagua kuwaongoza Kampeni za kuwachagua wakurugenzi wa almashauri ya maendeleo ma majani chai nchini KTDA.
Katika kikao na wanahabari katika kituo cha ukusanyaji na upimaji zao la chai eneo la Bomondo Nyamira mjini baadhi ya wakulima hao wamewashauri wakaazi wanaokuza majani chai eneo hilo kutoshawishika kwa vyovyote vile kuwachagua viongozi wasiofaa kwani kulingana nao viongozi wasiofaa kunachangia mapato ya chini kwa wakulima.
Imetayarishwa na Janice Marete