RUTO AVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI
Rais William Ruto amevunja baraza lake la mawaziri na kuwafuta mawaziri wake wote pamoja na mwanasheria mkuu Justin Muturi na kutakiwa kuondoka afisini mara moja.
Akizungumza katika hotuba kwa taifa muda mfupi uliopita, Ruto amesema afisi ya pekee itakayosazwa na ile ya Naibu wake na mkuu wa mawaziri.
Rais amesema amechukua uamuzi huo kufuatia malalamishi ya Wakenya.
Aidha, rais ameahidi kufanya mashauriano ili kubuni kikosiu kitakachomsaidia kuafikia malengo ya serikali yake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































