#Local News

MAHAKAMA KUU YAKATAA KUSITISHA MCHAKATO WA KUMUONDOA GACHAGUA

Mahakama kuu kwa mara ya pili imekataa kutoa amri ya kusitisha kesi ya kumtimua mamlakani Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Kesi hiyo imetajwa mbele ya Jaji Bahati Mwamuye, ambaye ameagiza shauri lililowasilishwa na Cleopas Malalah lifikishwe mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita kwa maelekezo zaidi.

Wakati huo huo katika ombi la kutaka maswala yote ya kupinga mchakato wa mashtaka kuunganishwa, Bunge linasema kuwa masuala hayo yanaibua masuala sawa na yanapaswa kuunganishwa ili kuhojiwa na Mahakama ili kuendeleza uondoaji wa Malalamiko kwa ufanisi na haraka.

Mnamo Septemba 30, mahakama ilikataa kutoa maagizo ya kusitisha Bunge kushughulikia ombi la kuondolewa mashtaka dhidi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Hoja iliyowasilishwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala ililenga kuzuia Bunge la Kitaifa na Seneti kuwasilisha, kujadili, kuzingatia au kufanyia kazi hoja yoyote ya kutaka kumtimua DP Gachagua.

Malala alisema kuwa mabunge yote mawili hayana kikomo kinachohitajika cha kanuni ya kijinsia ya theluthi mbili na hivyo yamekiuka masharti ya Katiba.

Imetayarishwa na Janice Marete

MAHAKAMA KUU YAKATAA KUSITISHA MCHAKATO WA KUMUONDOA GACHAGUA

BARAZA LA MAGAVANA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA LEO

MAHAKAMA KUU YAKATAA KUSITISHA MCHAKATO WA KUMUONDOA GACHAGUA

DIANA GICHENGO :RUTO AMEKIUKA KATIBA, HOJA YAKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *