WANNE WANASWA KWENYE MSAKO WA POMBE HARAMU THARAKA NITHI
Polisi huko Tharaka Nithi wanazuilia washukiwa 4 walionaswa wakati wa msako dhidi ya pombe haramu na dawa nyingine za kulevywa katika soko la Kibunga.
Wanne hao walipatikana na lita 200 za pombe na misokoto 31 ya dawa za kulevywa aina ya bangi na sasa wanasubiri kufikishwa kotini siku ya jumatatu.
Idara ya usalama sehemu hiyo imetaka ushirikiano wa wakaazi katika kufichua wanaoendeleza biashara ya kutengeneza na kuuza pombe haramu.
Imetayarishwa na Maureen Mukhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































